JE UKIWA NA JANABA NA HEDHI UTASOMA QUR`AANI NA KUKAA MSIKITINI

May 7, 2008 / by www.maduru

   NI UPI UBAINIFU WETU KUHUSU JANABA,HEDHI NA NIFASI?

        Bila shaka suala la janaba,hedhi na nifasi wanazuoni wote wamekubaliana kuwa ni haramu kuswali,lakini ni halali kufunga saumu kwa mwenye janaba iwapo atajimai kabla ya alfajiri au akaota ndoto ya kujimai mchana wa funga,na ni haramu kwa mwenye hedhi na nifasi,na vilevile  hawakukhitalafiana namna ya kujitoharisha.Isipokuwa suala la kuingia msikitini,kusoma qur`aani na kuchukuwa masahafu kila kundi lina muono tofauti kwa jinsi walivyoielewa Qur`aani na sunnah.Hivyo kwa faida ya msomaji apendae dini yake na akitaka kuelewa-Jambo hili tumejitahidi kubainisha miongoni mwa hadithi chache katika mafungu yafuataya  

a)      Hoja zitumiwazo kukataza kusoma Qur`aani na kuichukuwa.

b)      Hoja zitumiwazo kuruhusu kusoma Qur`aani na kuichukuwa.

c)      Hoja zitumiwa kuruhusu kukaa msikitini.

d)      Hoja zitumiwazo kukataza kukaa msikitini.

e)      Hoja ya usahihi au udhaifu wa hadithi katika mafungu hayo

 

(a)Hoja zitumiwazo kukataza kusoma Qur`aani na kuichukuwa:

1) Kutoka kwa Ally (r,a) ilikuwa hakuna kitu kilichokuwa kinamzui mtume (s.a.w) kusoma Qur`aani isipokuwa                                                                                                                                                                                  janaba,(wamepokeya maimamu wa wa sunnah,na imaamu Tirmidhi akaisahihisha)

Kutoka kwa  Ally (r,a) anasema nilimuona mtume (saw) akitawadha kisha akasema,namna hii ni kwa asie na   janaba………..(Imaam Ahmad na Abuu Yaala)

(b) Hoja zitumiwazo kuruhusu kusoma Qur`aan na kuichukuwa:

       1)     Kutoka kwa Aisha (r.a) alikuwa mtume (s.a.w) akimdhukuru Alla (s,w) katika kila hali zote (Muslim na

               Abuu Yaal)               

       2) Mtume (s.a.w) alipeleka barua kwa Hirkila akimtaka asilimu kwa kumuandikia:-Bismillahir rahmaanir

            rahiim-Sema uwaambie watu wa kitabu njooni katika neno lililo sawa baina yenu na baina yetu,ya kwamba

            tusimwabudu yeyote ila Allah (s,w) wala tusimshirikishe na chochote: wala baadhi yenu tusiwafanye

           wengine kuwa mungu badala ya Allah (s.w) wakingeuka semeni: shuhudieni ya kwamba sisi ni waislam.

           (3:64)  Hivyo basi Imaam Bukhari,Twabaraaniyyu,Abuu Daudi na Ibn Hazim wakajuzisha kwa kuona si

           vibaya kwa mwenye hedhi na janaba kusoma na kugusa msahafu,kutokana na rai hii hata ibn Abbaasi

           hakuona ubaya kutokana na hadithi iliyopo katika kifungu (b) hadithi namba (1)

©Hoja zitumiwazo kukataza kukaa msikitini:

  1)  Hakika msikiti si halali kwa mwenye hedhi na janaba (ibn Majah na Twabaraani)

(d)Hoja zitumiwazo kuruhusu kukaa msikitini:

1)      Na ilikuwa mmoja wetu akipita msikitini hali akiwa na janaba (Abi Shaibah na Saad ibn Mansuur)

2)      Kutoka kwa Aisha (r,a) amesema  aliniambia mtume (s.a.w) nilete  kilemba kilichopa  msikitini,Aisha akajibu mie nipo hedhini,akasema mtume (s,a,w) hedhi haipo mikononi mwako (Maimamu wa sunnah ila Bukhari)

3)      Kutoka kwa Maimuna (r,a) amesema,alikuwa mtume (s,a,w) akiingia kwa mmoja wetu hali tukiwa na hedhi  na akiweka kichwa chake katika paja la mmoja wetu na huku akisoma Qur`aan kishaa anasimama mmoja wetu na kuweka kilemba msikitini akiwa hedhini.

4)      Kutoka kwa Atwaai ibn Yasaar amesema nimewaona watu katika masahaba wa Mtume (s,a,w) wakikaa msikitini wakiwa na janaba pindi wakitawadha udhu wa salah (isnadiye ni sahihi kwa sharti la Imaam Musilm).          

e)Hoja ya usahihi au udhaifu wa hadithi katika mafungu yote:

      1)  Sheikh Nasoro din Albaan katika hoja fungu © hadithi namba 1amesema wapokezi wake hawakuthibitika

           katika uhifadhi wao, na aksema Imaam Bukhari hiyo ni hadithi yenye kushangaza,na amesema Imaam

           Khitwaabiyyu kuwa wanazuoni wengi wameidhoofisha hadithi hiyo, na amesema Baihaqi hiyo hadithi haina

           nguvu, na amesema ibn Hazim kwa kuenda mbali mno kwa kusema hadithi hiyo ni batili,na vile vile Imaam

           Ahmad na Muzanna wameidhoofisha kwa sababu wapokezi wake wameponyoka na hawafahamiki na

           akasherehesha sura ya 4:43 kuwa wapita njia ni wasafiri waliofikwa na janaba wakakosa maji wanastahiki

           kutayammamu na kuswali kama ilivyopokelewa na ibn Abbaas.

     2)   Katika hoja ya fungu (a)hadithi namba 2 sheikh Nasoro Din Albaani ameziweka katika mafungu mawili ya

           udhaifu na mauquufu, na katika udhaifu ni kama alivyothibitisha Imaam Al-hafidhi ibn Hajar, na kwa  

           upande

        wa mauquufu ametolea hoja Imaam  Daarqutwiniyyu na wengineo,na vilele imewekwa wazi kwa udhaifu wa

        hadithi hiyo katika sunani ya Abuu Daudi ukurasa wa 31.Maelezo haya yanapatikana katika kitabu cha Fiqih

        sunnah cha Sheikh Said Sabiq na Tamaaml minna cha Sheikh Nassoro Din Albaani na tafsiiri ya Qur`aani ya

        ibn Kathiir sura ya 4:43

   Ndugu waislam miongoni mwa matatizo makubwa yanayokabili umma wa kiislam ni kuwa masheikh zetu mara nyingi hawepindi kuweka wazi hoja za madhehebu yote manne yenye kutegemewa, ili waislam wakabainishiwa hoja ili wao wenyewe wakawa waamuzi  (majaji).Pia maimam wote wanne msimamo wao juu yamas`ala yenye khitlafu wanasema ikisihi hadithi hayo ndio madhehebu yao.Mashekhe wetu wa leo iwapo kama watachukuwa hekima kama ya aliyekuwa sheikhe wetu wa mkoa mar`uum Mohammed Shaibu- Allah amrehemu alipoulizawa:Hivi  sheikh uzikaji upi ulio sahihi kati ya tahlili na kimya-kimya? Akajibu kimya-kimya ni katika hadithi ya Mtume (s,a,w) lakini wanazuoni wakaweka tahlili kwa sababu zama hizi binadamu hawaheshimu misingi ya dini na lengo kuu ni kuwafanya watu wote wasiongee wakati wa jeneza linapelekwa makaburini-Alhamdulillah ni Busara iliyoje na Heshima iliyoje kwa wanazuoni wenye kujuwa wajibu wao kwa sababu wao wamepewa dhimma na Allah (s,w) ya kuongoza umma.Hakika sisi sote ni wa mwenyezi mungu na kwake ni matrejeo yetu.

WABILLAH TAWFIQ    ALLAH AALAM

0 comments on JE UKIWA NA JANABA NA HEDHI UTASOMA QUR`AANI NA KUKAA MSIKITINI

Add a comment

To add comments without entering your email and image verification, you must be logged in. Login or Join Blogster

  • Type the words in the box below the image.

Email this blog post to a friend

To email posts to friends, you must be logged in. Login or Join Blogster

Friends

www.maduru currently has no Blogster friends

Add him as a friend and send him a friendly welcome!