KHUTBA YA KUAGA YA MTUME (SAW)
Khutba hii ilitolewa na mtume Muahammad (SAW) tarehe 09 Dhul Hijja mwaka wa 10 Hijriya kwenye milima ya Arafah huko makkah-Saudia Arabia-alipokwenda mtume (SAW) kufanya ibada ya Hijja ambayo pia ilijulikana kama Hijja ya kuaga.
Baada ya kumshukuru Allah (SWT) na kumsifu,mtume (SAW0) alianza khutba kwa kusema:
Enyi watu!Nisikilizeni maneno yangu vizuri, kwani sidhani kama baada ya mwaka huu nitakuwa pamoja nanyi.Hivyo sikilizeni kwa makini nitakayoyasema na (maneno haya) mfikishieni kila asiekuwepo hapa leo.”
“Enyi watu! Hakika damu zenu na mali zenu ni takatifu kwenu kama mlivyoufanya mwezi huu kuwa mtakatifu na mji huu kuwa mtukufu.”
Rudisheni amana mlizokabidhiwa kwa wenyewe wanaostahiki.Msimdhuru yeyote ili nanyi msije mkadhulumiwa. Kumbukeni mtakuja kukutana na mola wenu naye atahesabu amali zenu.Allah (SWT) amekukatazeni kula riba. Hivyo riba zote zimeondoshwa na mna haki ya kubaki na rasilimali (mitaji) yenu Hamna haki ya kudhulumu wala kudhulumiwa. Alla(SWT) ameharamisha riba na riba zote za Abbasi ibn Abdul Muttallib zimeondoshwa “
Kila haki ya kisasi iliyokuwepo enzi za Ujahiliya imefutwa na haki ya kwanza kuifuta ni ya Rabian ibn Harith ibn Abdul Muttalib”
“Enyi watu washirikina wanajaribu kuakhirisha (kuchelewesha) kalenda ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyoitukuza Allah (SWT) na kulifanya halali jambo ambalo Allah (SWT) ameliharamisha na kulikataza jambo ambalo Allah (STW) ameliruhusu.Miezi kwa Allah (SWT) ni kumi na miwili.minne kati yao ni mitakatifu,mitatu ikiambatana (Dhul Qaada) Dhul Hijja na Muharramu) na mmoja (Rajabu) uko kati ya Jumada (ya mwanzo na ya mwisho) na shaabani.
“Jiepuheni na shetani kwa ajili ya kuilinda dini yenu.Tayari (shetani) amekata tamaa kwamba ataweza kuabudiwa katika ardhi hii milele lakini bado ana mikakati ya ya kukupotezeni hivyo tahadhalini nae katika mambo mengine.”
“Enyi watu !ni kweli mna haki juu ya wanawake na wao pia wana haki juu yenu. Kumbukeni mmewachukuwa kuwafanya wake zenu kwa amana ya Allah (SWT) na mmehahalalishwa (kustarehe) nao kwa neno lake”.
‘Ninakuusieni kuwatendea wema wanawake na kuwa na huruma kwao kwani ni wake zenu na wasaidizi wenu. Ni haki yenu kuhakikisha hawafanyi urafiki na musiyemuhafiki na juu yao kutokufanya jambo la uchafu lililo wazi na pindipo wakifanya Allah amewapa idhini ya kuwahama kwenye malazi na kuwapiga kipigo kisichoumiza.Ikiwa watatekeleza majukumu yao basi na wao watakuwa na haki ya kulishwa na kuvishwa na kwa wema.”
“Enyi watu, nisikilizeni kwa utulivu, mcheni Allah (SWT), msali sala tano kila siku, fungeni katika mfungo wa Ramadhani na toeni zakah. Tekelezeni ibada ya Hijjah ikiwa mna uwezo.”
“Binadamu wote wametokana na Adamu na Hawa, hakuna mbora kati ya mwarabu na asiyekuwa mwarabu,wala asiyekuwa mwarabu kwa mwarabu,wala mweusi kwa mweusi au mweusi kwa mweupe isipokuwa kwa taqwa (kumcha Allah).
“Eleweni
Kila muislamu ni ndugu kwa muislamu na waislamu wote ni ndugu.Hatohalalishiwa muislamu na kitu chochote isipokuwa kila alichopewa kwa ridhaa na ndugu yake. Wala msidhulumu nafsi zenu.Na msisahau kwamba kuna siku mtakutana na mola wenu na mtahesabiwa amali zenu. Hivyo tahadhalini msije mkapotea baada yangu”
“Enyi watu! Hakuna tena Mtume baada yangu na hakuna dini nyingine itakayo kuja.Ninakuachieni vitu viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea milele navyo ni QUR`AANI na SUNNAH (mwenendo) wangu”
“Wale wote walionisikiliza waufikishe ujumbe huu kwa wengine, na wengine waufikishe kwa watakaofuata na inawezekana hawa wa mwisho wakayafahamu vyema maneno yangu kuliko hawa walionisikiliza moja kwa moja.”
“Ewe mola shuhudia kwamba nimefikisha ujumbe kwa watu wako”
Kila
Nikiisoma khutba hii huhisi kama imetolewa jana wakati ni karne kumi na nne na thuluthi (miaka 1427) tayari zimepita. Kila nikiisoma khutba hii huyatafakari tena maneno haya machache ya Mtume (SAW) lakini yamejaa mafundisho na kusheheni hazina ya elimu na mausio.Khutba iliyokusudiwa waislamu wote duniani popote walipo,Kizazi baada ya kizazi,karne baada ya karne. Ni wasia ambao ametuagiza Mtume (SAW) tuufikishe kwa kila muislamu.Ndugu zangu wailamu, Hazina kama hizi ndizo tulizoagizwa kufikishiana.Inshaallah kila atakaepata ujumbe huu ahakikishe anamfikishia mwengine kama tulivyoagizwa na Al Habib Mustafa (SAW) na sasa inawezekana miongoni mwetu kuwapata utakaomsikiliza Mtume (SAW) na kumfahamu vyema na hivyo kuufuata mwenendo wake.
Tumoumbe Allah (SWT) atujaalie miongoni mwao.
Aamin.
0 comments on KHUTBA YA KUAGA YA MTUME (SAW)
Add a comment
To add comments without entering your email and image verification, you must be logged in. Login or Join Blogster