BISMILLAHIR RAHMAANIR RAHIYM
NI WAPI TUNAPOKOSEA??
Enyi binadamu hakika dini ya uislam ni mfumo wa maisha au utaratibu wa maisha ambao mwenyezi mungu (S.W) amemuamrisha binadamu aufuate ili apitishe maisha juu ya mfumo huo.na wala si kama anakomolewa au kutaabishwa laah hasha bali apate maisha ya furaha na amani kuliko mifumo yote anayoifuata ambayo imeratibiwa na fikra za binadamu (mabunge) ambayo ina udhaifu na mapungufu makubwa yanayopelekea kufanywa marekebisho kila baada muda Fulani
Ewe binadamu jambo lolote katika uislamu liwe dogo au kubwa lina umuhimu mkubwa na maslahi ya binadamu katika maisha.Kwa mfano tukizingatia maamrisho ya mtume wa mwenyezi mungu (S.W) ya kuwatembelea wagonjwa mahosptarini au majumbani kwa kutambua hali zao, hapa kuna mafundisho ya msingi na wala sio kutalii katika mawodi na kuwaangalia kama picha, laah hasha bali ni kuwapa subra.kuwasaidia na kuwaombea dua kwa mtihani walioupata kama alivyopokea Abuu Hurairah (R.A) kutoka kwa Mtume (S.A.W) kuwa Mwenyezi mungu (S.W) atasema siku ya kiyama ;Ewe binadamu! Nilikuwa mgonjwa wewe hukunitembeleya! Atasema: Ewe mola wangu! Nitakutembeleaje ilhali wewe ni mola wa walimwengu? Atasema: Je hujuwi mja wangu Fulani alishikwa na ugonjwa lakini wewe hukumtembeleya kuulizia hali yake .Je hujuwi kama ungemtembeleya ungalinikuta huko Karibu yake? Ewe mwanadamu! Nilikuomba chakula lakini wewe hukunilisha.Atasema :Ewe mola wangu! Nitawezaje kukulisha ilhali wewe ni muumba wa ulimwengu na ni mola wa ulimwengu? Atasema:Je hukuwa na habari Mja wangu fulani alikuomba kumlisha lakini wewe hukumlisha! Je huna habari ungemlisha ungelinikuta mimi Karibu yake? Ewe mwanadamu! Nilikuomba kinywaji lakini wewe hukunipa mimi kinywaji! Atasema: Ewe mola wangu! Nitawezaje kukunywesha hali wewe ni mola wa ulimwengu? Atasema mja wangu fulani alikuomba kinywaji lakini wewe hukumpa kinywaji. Je huna habari kama ungempa kinywaji ungelinikuta mimi huko Karibu yake? (muslim) kutokana maelzo ya hadithi hiyo yatosha kufahamu uislamu sio dini ya malipo akhera tu kama inavyo chukuliwa na makundi ya watu wengi wakiwemo waislamu wenyewe, laah hasha!! bali uislamu ni dini iliyoangalia kwa upana na marefu katika maisha ya kijamii ambayo yanampelekeya binadamu aishi katika duniya hii kwa furaha bila ya matatizo makubwa wala khofu ya kumfadhahisha kama alivyobainisha hivyo Allah (S.W) “Tuliwaambiya teremkeni katika ardhi nyote,na kama ukikufikieni kutoka kwangu uongofu (Quraani na sunnah) atakayefuata uongofu wangu hakuna khofu juu yao wala hawatahuzunika” (Quraani 2:38) na tuzingatie kwa makini kwa makini hadithi aliyopokeya Ali (R,A) kutoka kwa mtume (S.A.W) kuwa:”Muislamu anapomtembeleya muislam mgonjwa kwa kuulizia hali yake wakati wa asubuhi malaika elfu sabini huenda kumuombea baraka mpaka usiku:Na kama amekwenda kumtazama wakati wa usiku malaika elfu sabini humsalia mpaka asubuhi na hupewa bustani yenye matunda ya peponi” (Tirmidhi.)Je ahadi hii ya pepo katika dini ya uislamu ni kama ya kikristo kwa kufuata mambo mepesi na yasiyokuwa na gharama na kuamini kuwa Yesu kristo amesurubiwa kwa dhambi za wakristo na mkristo anasubiri kuponda raha ya uzima wa milele na sisi tunasubiri bustani ya miti ya peponi kwa kufanya utalii kwa wagonjwa
Enyi waislamu kwa kutozingatia mafundisho yaliyomo katika kitabu cha Allah S.W na sunnah za mtume (S.A.W) leo uislamu unaonekana kama dini ya ubabaishaji na isiyokuwa na dira,na wale wanaoifuata kuwa madhalili mbele ya makafiri ni kwa sababu sisi waislamu wenyewe tumeamua kwa makusudi kwa kufuata baadhi tu ya mafundisho ya Quraani na Sunnah na zao la hilo ni fedheha ya waislamu ndani ulimwengu kama Allah (S.W) anavyothibitisha hilo katika Quraani kuwa ”Je munaamini baadhi ya kitabu na munaacha baadhi yake hakuna malipo kwa afanyaye hayo katika nyinyi ila ni fedheha katika maisha ya duniya na siku ya kiyama mutarudishwa katika adhabu kari kabisa na mwenyezimungu si mwenye kughafirika kwa hayo munayoyafanya: (Quraani 2:85)
Enyi ndugu waislamu asili ya uislamu ni utaratibu unaolingana na maumbile ya binadamu kama Allah (S.W) anavyothibitisha hilo pale aliposema “Basi elekeza uso wako kwa dini iliyo sawa sawa ndilo umbile mwenyezi mungu aliloumbia watu.Hakuna mabadiliko katika dini ya mwenyezi mungu (S.W.)Hiyo ndio dini iliyo ya haki, lakini watu wengi hawajui:” (Quraan 21:30) Hivyo waliotutangulia miongoni mwa masahaba watukufu jinsi walivyokiishi katika jamii iliwapelekea hata wasiokua waislamu kuingia katika uislamu bila ya kuwahubilia,Je leo hii sisi waislamu tunaochagua kwa kufuata mafundisho baadhi na mengine kuyaacha,na isitoshe kibaya zaidi waislamu wenyewe kwa makusudi wameamua kuzifanyia istihizahi (kebehi) baadhi ya Aya za Quraan na Sunnah za Mtume (S.A.W) ,je ni kweli tupo katika uislamu kamili kama aliokusudia Allah (S.W) au tunayaabudu matamanio yetu kama anavyotusemanga mwenyezimungu (S.W) kwa kusema “Je umemuona anayefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake je wewe unaweza kuwa mlinzi juu yake” Quraan 25:43 Je ndugu waislamu ni lipi tumaini letu mbele ya mwenyezimungu (S.W.)?
0 comments on NI WAPI TULIPOKOSEA
Add a comment
To add comments without entering your email and image verification, you must be logged in. Login or Join Blogster