BISMILLAHIR RAHMAANIR RAHIYM
UFAFANUZI WA SALA YA JAMAA ZAIDI YA MOJA KATIKA MSIKITI WENYE IMAAM MAALUM.
Hakika Mtume (saw) siku moja alikuwa pembeni mwa mji wa Madina alipofika msikitini akakuta watu wameshasali akaelekea nyumbani na akasali jamaa na watu wa nyumbani kwake.(Amepokea Twabari katika kitabu muujamul likabiiru na kitabu cha Austawi na akaisahihisha Sheikh Albaani)
Hakika Alkamah na Aswad walifika pamoja na ibn Masuudi (r,a) katika msikiti wakakuta watu wameshasali.Ibn Masuud (r.a) akarudi nao mpaka nyumbani kwao na kuswali nao,(Amepokea Abdul Razak katika kitabu Muswannif juzuu ya 2 ukurasa wa 409 na Imaam Twabar katika kitabu cha Muujamul kabiiru juzuu ya 9 ukurasa wa 318.)
Na amesema Imaam Shaafi,na ikiwa katika msikiti kuna Imaamu maalum, na ikiwa mtu au watu wamechelewa na imewakosa sala ya jamaa! Basi waswali kila mtu peke yake.Mie sipendi watu waswali jamaa ya pili, na wakifanya hivyo itajuzu sala (jamaa) na bila shaka itakuwa karaha kwa jamaa hiyo kwa sababu hawakufanya wema wetu waliotangulia (Masahaba na Taabigh) haya yamo katika kitabu cha (Al-ummu cha Imaam shaafi.)
Na amesema Abu Hanifa haijuzu kurudiwa salah ya jamaa katika msikiti wenye Imaamu na mfano wa maelezo hayo vilevile ameeleza Imaamu Maaliki katika kitabu cha Maduunati (kama alivyonukuu sheikh Nassoro din Albaani katika Tamaamul liminna)
Siku moja alikuja Mtume (saw) pamoja na baadhi ya masahaba na ikawa sala imeshasaliwa na wakasali kila mmoja peke yake ,hadithi hipo katika (kitabul Al-ummu cha Imaamu Shaafi)
Ndugu waumini hizo ni baadhi ya ushahidi kutoka kwa Mtume mwenyewe pamoja na Masahaba, na ndio maana Imaam Shaafi ni miongoni mwa maimamu wanne wakubwa alipata nguvu ya kutamka ni karaha kuendeleza jamaa ya pili katika msikiti wa Imaamu maalumu,kwa sababu watu watapuuza sala ya jamaa kuu kwa makusudi na kujiwekea vijijamaa vya kiholela na yatakosekana makusudio ya umoja wa waislamu katika harakati zao za kusimamisha uislamu katika jamii.Kwani ikumbukwe miongoni mwa makusudio ya salah ya jamaa ni kupeana majukumu au taarifa muhimu, hivyo ndio maana jamaa mbili haikuwekwa hata katika salah ya khofu na Mtume (saw) aliweka kanuni maalumu jinsi ya kuisali sala ya khofu.Na Mtume (saw) kwa kusisitiza yule ambaye imemkosa sala ya jamaa kwa udhuru kwa kusema: Ataetawadha vizuri udhu wake kisha akaenda msikitini na akakuta watu wamesha Sali,Basi Allah (swt) atampa malipo ya mfano wa aliesali sala ya jamaa na bila ya kupunguziwa chochote wale waliosali sala ya jamaa.(Amepokea Abuu Daud,Annasaai,Ahmad, Bukhari na Hakim)
Ndugu waislam hayakupatikana haya ya kujiwekea vijijamaa vingi misikitini isipokuwa katika karne ya saba kama ilivyo wekwa wazi katika kitabu cha (Fatihil lialaa juzuu ya 1 ukurasa wa 92).
WABILLAH TAWFIQ
ALLAH AALAM.
0 comments on UFAFANUZI WA SALA YA JAMAA ZAIDI YA MOJA KATIKA MSIKITI WENYE IMAAM MAALUM.
Add a comment
To add comments without entering your email and image verification, you must be logged in. Login or Join Blogster