BISMILLAHIR RHMAANIR RHYIM
ENYI WASLAMU JIFUNGENI NA HUKMU ZA KISHERIA WALA MUSISHIRIKI KATIKA KURA CHINI YA NIDHAMU YA KIILMANIYYA KIDEMOKRASIA ILIOBUNIWA JUU YA UKAFIRI
Mwezi Disemba 2007 kunatarajiwa kutokea uchaguzi mkuu wa kumi, na tayari wimbo wa demokrasia wa vyama vingi wasikika kote nchini, wakati huo huo badhi ya waislamu na makundi yao yanayodai kuzungumza kwa niaba ya waislamu wamewaunga mkono wagombeaji fulani na vyama vyao, hata kama wagombeaji hao si waislamu kuzidisha mambo utata baadhi yao wanahamasisha waislam kufikia kiwango cha kudai kuwa eti kupiga kura ni jihadi na ni wajibu wa kidini. Ni muhimu kwa waislamu wacha mungu kutambua hali halisi ya kidemokrasia ya vyama vingi kabla kuambatanisha na dalili za kisheria zilizowazi, na kwa mujibu wake wajifunge na hukmu za kisheria bila ya kujali maslahi yake ya kibinafsi.
Demokrasia ni nidhamu ya kiutawala ya kimagharibi iliyobuniwa juu ya itikadi ya Kiilmaniyya, Mayunani wa zama za kale ndio wa mwanzo waliozua agenda hiyo kasha baadaye ikahusishwa upya katika mapinduzi yaliyotokea ufaransa mwaka 1789 na kunukuliwa katika katiba ya Amerika mwaka 1776. Ilmaniyya humaanisha binadamu atenganishe dini yake na maisha yake, na dini ibakie kuwa ibada chache zinazofungika katika majumba ya ibada bila ya kuwa na usemi wowote au muongozo kwa yale yanayojili nje ya majumba ya ibada. Ilmaniyya [secularism] latokana na tamko la `kiyanuni` Linalomaanisha kilichoko nje ya hekalu [jumba la ibada ]mfano mambo yanayohusu mahusiano baina ya mke na mume, katiba, ukadhi, uchumi n,k ambapo mtu hupewa ruhusa ya kuendesha maisha yake kwa matamanio yake kwa mujibu ya kanuni zilizotungwa na wanadamu bila ya kujali muongozo wa kidini, akhlaqi au mila.
Kwa hivyo sheria ya muumba hufungwa ndani ya majumba ya ibada, huku mwanadamu akijitweka ubwana wa yale yaliyo nje yake. Demokrasia linatokamana na matamko mawili ya kiyunani [demos kratos] kwa maana utawala kwa watu ambao maana yake ni watu wanamiliki ubwana kamili na uhuru usiokuwa na vikwazo wa kutunga sheria ili kupeleka maisha yao, kazi ambayo haimstahiki ila muumba. Ndio utayaona mabunge yote ulimwenguni yakihalalisha yale aliyoyaharamisha allah kwa njia ya kukatikiwa kama kumtukana mtume [saw] kamari, tiba, zinaa, tembo, kumtawaza kafiri kama mtawala wa waislamu n,k na wakati huo huo huharamisha yale aliyoyafaradhisha Allah kwa njia ya kukatikiwa kama kuvaa hijab, kulingania umoja wa ummah chini ya serikali ya khilafah, kupigana jihad n.k.
Enyi waislamu dalili za kisheria ziko wazi katika kukufurisha itikadi ya kiilmaniyya na matunda yake ya demokrasia na uhuru n,k. aqeeda ya kiislamu imedhihirisha wazi kuwa ubwana ni wa allah [swt] peke yake bila ya kushirikishwa na yeyote na sheria yake ndio yenye kutawala nyanja zote maishani, sawa sawa ndani ya msikiti au nje yake, Asema Ta`ala:
Hakuna hukumu ila ya Allah(tu) (Yusufu:40) Na asema Taala: Naapa kwa mola wako miezi hawajaamini [kikweli ] mpaka wakufanya [wewe ndiye ] hakimu katika yale wanayo khitalafiana, kasha wasione uzito nyoyoni juu ya hukmu uliyoitoa na wanyenyekee kikamilifu [tmq 4: 63]
Haifai kata kata kwa muislamu yeyote kukubali mwito wa kikafiri wa ki ilmaniyya na nidhamu ya kidemokrasia inayomruhusu mwanadamu kutunga sheria na kupuuza sheria ya Allah Asemaa Ta`ala Haiwi kwa muumini wa kiume wala wa kike pindi Allah na mtume wake wanapo kata shauri wawe na hiari katika shauri [tmq al ahzaab
36] Allah [swt] ameteremsha dini kamili ya kiislamu yenye hukmu katika kila nyanja ya maisha iwe katika ibaadat,uchumi,siasa,katiba akhlaqi n,k ili kumuongoza muislam katika mambo yake yote na sheria ya kiislam pasina kuwa na khiyari ya kutunga sheria zake mwenyewe Asema ta`alah:
Na tumekutelemshia kitabu kielezacho kila kitu na Asema taalah:
Leo nimekukamilishieni Dini yenu na kukutimizieni neema yangu, na nimeridhika uislam kuwa ndio dini yenu pekee(Almaidah) Kafiri pekee ndiye anayeweza kuchagua hukmu ya kidhulma na kijahiyya zilizotungwa na wanadamu haya ya sheria ya allah [swt] anasema ta`ala
Hao wanataka hukmu za kijahiliyya na ni nani aliye mwema zaidi katika hukmu kuliko allah [yanayofahamika haya] na watu wenye yakini [tmq al maidah 50] anasema ta`ala:
uwaoni wale wanaodai kwamba wanaamini yale yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyotelemshwa kabla yake? na wanataka kuhukumiwa kwa twaghuti [njia isiyowafiki sheria]hali wameamrishwa kukana twaghuti [tmq an nisaa 60]
Enyi waislamu tahadharini nakila mwenye kuwalingania, aidha kimakusudi au kwa kutojua, kushiriki katika uchaguzi kwenye nidhamu ya ki ilmaniyya ya kidemokrasia kwani huyo anawalingania kwenye ukafiri. Juu ya hayo yawalingania musimame pamoja namaadui zetu wamagharibi wa wa-koloni wa ki-misalaba wakiongozwa na Amerika wanaopiga vita biladi za kiislamu ili kutabikisha kwa nguvu nidhamu ya ki-ilmaniya ya kidemokrasia mabadiliko kwa mfumo wa kiislamu na nidhamu yake ya utawala yaani
Al-khilafah Ar-rashida.
Enyi waislamu jifungeni na aqeedah sahihi ya kiislamu na mwenendo wa bwana mtume [saw] katika kulingania uislamu kama mfumo kamili wa kimaisha bila ya kushawishika kushiriki katika nidhamu ya kikafiri. waislamu wa Kenya lazima wajifunze kutokana na makosa ya ndugu zao huko Algeria, Misri, Palestina na wenginepo waliojaribu kutabikisha uislamu kupitia kushiriki katika uchaguzi wa ki ilmaniyya wa kidemokrasia iliyowatia katika mtego wa nidhamu uliotaka imma kuwatumia kwa ajili yamaslahi ya ukafiri au kuwakatisha tama. Allah alimtahadhalisha mtume wake [saw] na mitego ya kikafiri huko makka, na tahadhali hiyo yatukusanya nasi mpaka leo pindi aliposema ta`ala
[makafiri ] wanapenda uwe laini [kwa kushiriki nidhamu zao ] nao watakuwa lini kwao [tmq al qalam:9 ] Lazima tumuagize Mtume(saw) aliyeishi katika Daar A-kufrn kama tunavyoishi sisi leo,hakusalimu amri bali alifanya bidii ili kubadilisha hali ya kuwalingania ulinganizi wa kimfumo wa kiislamu kama badili wa fisadi na umaskini unaoletwa na ukafiri,kupitia mvutano wa kifikra na mapanbano ya kisiasa bila ya kutumia nguvu. Huku akitumia ukweli na dalili za kiislamu zilizohujumu fikra na misingi ya nidhamu za kikafiri kiarabu zama hizo mpaka kufaulu kuusimamisha Uislamu kupitia dola Dola la kiislamu huko madina.
Ni madai ya urongo kuwa uislamu wasiposhiriki katika uchaguzi watapata madhara makubwa.Bali waislam walishirika chaguzi zote kutoka `uhuru`na kila mara walipata madhara makubwa yaliyosababisha na nidhamu za kifisadi.Isitoshe kuna jamii zisizokuwa za kiislam zinazoishi Kenya pasina uwakilisha wowote serikalini lakini zimeweza kufanikiwa katika kupeleka maisha yao kwa uchache kupata ufanisi hapa duniani.Amma waislamu lengo letu ni kumridhisha mola wetu hata kama tutapata taabu hapa duniani na ni jukumu letu kuubeba Uislamu kama mfumo badili ya uovu wa demokrasi ulioneza ufisadi,ukabila,ujinga na maradhi katika Afrika.
Ni urongo zaidi kudai kuwa waislamu wanawajibika kushiriki kwa ajili ya kisingizio cha `dharura`au `uovu ,Huo ni uwongo kwa sababu waislamu wa Maka zama za Mtume (saw) walikuwa wachache kiidadi na katika hali mbaya zaidi lakini hawakushiriki katika nidhamu za kikafiri pamoja na kudhulumiwa,kuteswa na hata baadhi yao kuuwawa!Bali walihiyari kufa shahidi kuliko kuuza uislamu wao huku wakijitahidi kutetea haki zao katika Daar Al-kufr pamoja na kudumu katika kutekeleza jukumu lao la kimsingi la kulingania Uislamu kama suluhisho la kudumu.Na kushiriki katika uchaguzi wa ki-ilmaniyya wa ki-demokrasia ni uovu mkubwa zaidi kwani ndio kuhalalisha ukafiri na kuupiga vita uislamu ambao ndio suluhusho pekee.
Enyi waislamu! Hizb ut-Tahrir Kenya waliwalingania katika mwezi wa huu Ramadhani kuungana nayo katika kujifunga na hukmu za kisheria na kukwepa mtego wa kushiriki katika nidhamu za ki-ilmaniyya ya ki-demokrasia huku tukifanya bidii kulingania Uislamu utakao eneza uadilifu na haki kote duniani pamoja na kukomboa ulimwengu kutokamana na ufisadi na maovu ya ukafiri. Asema Ta`ala:
Anachokupeni mtume, kichukuweni na anachowakanyeni nacho kiwacheni.Na mcheni Allah kwani Allah ni mkali wa kuadhibu (Qur Al-Hashir:7)
0 comments on UISLAMU NA DEMOKRASI
Add a comment
To add comments without entering your email and image verification, you must be logged in. Login or Join Blogster